Jumatatu 2 Juni 2025 - 17:55
Hawza ni zaidi ya mafunzo na kufundisha, ni kiongozi wa Mapinduzi ya Kifikra na Kimaadili

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Aqil al-Gharawi, katika hotuba yake, alibainisha kwamba Hawza si kituo cha masomo tu, bali ni chimbuko la mapinduzi ya kifikra na kimaadili, walimu wanapaswa kuweka kipaumbele cha juu katika kulea fikra na maadili ya wanafunzi.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, hafla ya iliyofana iliandaliwa kwa ajili ya kumbukumbu ya siku arobaini tangu kufariki kwa mwanachuoni maarufu na faqihi aliyeheshimika, Ayatollah Sayyid Muhammad Baqir Musawi Safawi (rehmatullah ‘alayh), katika Husayniyya ya mji wa Budgam, jimbo la Jammu na Kashmir. Katika hafla hiyo, Hujjatul-Islam Sayyid Aqil al-Gharawi, mmoja wa wanachuoni mashuhuri na wasomi wakubwa wa India, alitoa hotuba kuhusu mada ya "Elimu, Uendelevu na Ustawi wa Mwanadamu". Pamoja na kusisitiza nafasi ya kimkakati ya hawza katika kuunda na kuelekeza mabadiliko ya kifikra na kitamaduni katika jamii za Kiislamu, alifafanua daraja tukufu la elimu katika kumuinua mwanadamu.

Mwanachuoni Mashuhuri wa Kihindi: Hawza ni Zaidi ya Mafunzo na Kufundisha, Ni Kiongozi wa Mapinduzi ya Kifikra na Kimaadili

Aliongeza kuwa: Hawza si kituo cha kufundisha na kujifunza maandiko ya kidini pekee, bali ni ngome ya msingi kwa ajili ya kulea fikra, kuimarisha maadili, na kuweka misingi ya mapinduzi ya kitamaduni na kiroho katika jamii ya Kiislamu. Kutoka katika Hawza, fikra huibuliwa, mawazo hubadilishwa, na hatima za mataifa huamuliwa. Walimu wa Hawza wanapaswa kuiweka mstari wa mbele kazi ya kusafisha akili na kulea tabia za wanafunzi wao.

Katika sehemu ya mwisho ya kikao hicho, kulifanyika mkutano wa kitaaluma uliowashirikisha Hujjatul-Islam Aqil al-Gharawi, walimu wa Hawza na kundi la wanachuoni wa eneo hilo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha